Sio Mwakarobo Tena, Simba SC Yatinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF 2024/25
Kipa Mussa Camara aliibuka shujaa katika changamoto ya mikwaju ya penati akiokoa penati mbili kati ya tatu zilizopigwa na Al Masry
HABARI ZA MICHEZO
4/10/2025


Klabu ya Simba SC imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF msimu wa 2024/25 baada ya kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya Al Masry ya Misri katika hatua ya robo fainali.
Katika mechi ya kwanza ya robo fainali iliyochezwa katika dimba la New Suez Stadium, Misri, Simba SC ilipoteza kwa kufungwa magoli 2 – 0, magoli ya Al Masry yakifungwa na Abderrahim Deghmoum katika dakika ya 16 tu ya mchezo, huku John Okoye Ebuka akifunga goli ya pili katika dakika ya 89.
Katika mchezo wa marudiano uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam, Simba SC ilihitaji ushindi magoli matatu ili kuwawezesha kufuzu hatua inayofuata, au 2 – 0 ili kuwawezesha kwenda kwenye changamoto ya mikwaju ya penati.
Simba waliuanza mchezo kwa kasi ya hali ya juu, wakipeleka mashambulizi ya mara kwa mara katika lango la Al Masry na katika dakika ya 22 tu ya mchezo walijipatia goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wao Ellie Mpanzu, huku goli ya pili likifungwa na mshambuliaji Steven Mukwala dakika ya 32 kwa goli zuri la kichwa akiunganisha mpira uliopigwa na Mohammed Hussein.
Mpaka kwenda mapumziko Simba walikua tayari wanaongoza 2 – 0 huku wakiwa wametawala kila kitu kuhusu mchezo huo: Umiliki wa mpira Simba walikuwa na 73% huku Al Masry wakiwa na 27%, kona 8 kwa Simba huku wageni Al Masry wakiwa hawajapiga hata moja.
Kipa Mussa Camara aliibuka shujaa katika changamoto ya mikwaju ya penati akiokoa penati mbili kati ya tatu zilizopigwa na Al Masry, huku Jean Ahoua, Steven Mukwala, Kibu Denis na Shomari Kapombe wakifunga kwa upande wa Simba.
Mpinzani wa Simba SC katika Nusu Fainali
Katika hatua ya nusu fainali, Simba SC inatarajiwa kukutana na Stellenbosch FC ya Afrika Kusini. Stellenbosch FC imefuzu nusu fainali baada ya kuwafunga Zamalek SC ya Misri kwa ushindi wa jumla wa 1-0 katika robo fainali. Mchezo wa kwanza wa nusu fainali unatarajiwa kupigwa tarehe 20 mwezi huu jijini Dar Es Salaam huku mechi ya marudiano ikitarajiwa kuchezwa tarehe 26 pale Cape Town, Afrika Kusini.
Mashabiki wa Simba SC wanatarajia timu yao kuendelea na mwenendo mzuri na hatimaye kufuzu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF. Kocha Fadlu Davids na benchi lake la ufundi wanakabiliwa na kazi kubwa ya kuhakikisha wanajiandaa vyema kwa mechi hizi muhimu.
© 2024. All rights reserved.
Wasiliana Nasi
Tafadhali tujulishe kuhusu maswali au maoni yako
Vigezo na Masharti vitazingatiwa kwa ofa zote na bonasi zitakazotangazwa kwenye tovuti hii. Tembelea kampuni ya betting husika kwa maelezo zaidi. Sisi sio kampuni ya betting/mikeka na hatuchukui dau zozote. Odds za kipekee tunazotoa katika makala mahususi za habari ni za burudani na hazipatikani kwa kuwekewa dau. Kutumia taarifa yoyote inayopatikana katika www.mkekabetting.com kukiuka sheria yoyote ni marufuku. Angalia kanuni za bahati nasibu mtandaoni katika eneo lako la mamlaka kabla ya kuweka dau zozote na viungo vyovyote vya kutangaza mikeka.
Beti Kistaarabu
Hairuhusiwi chini ya miaka 18

