Hawa Hapa Wababe Waliotinga Nusu Fainali CAF 2024/25

Al Ahly, ambao wameweka rekodi ya kutinga Nusu Fainali mara sita mfululizo, wameendelea kuimarisha ubabe wao katika soka la Afrika kwani wamejipatika Clean Sheets 12 katika michezo 14

HABARI ZA MICHEZO

4/9/2025

Michuano ya Ligi ya Mabingwa Africa ‘CAF’ imeingia katika hatua za msisimko zaidi, na wababe wanne wa Afrika wameingia hatua ya nusu fainali.

Mamelodi Sundowns wamefanikiwa kutinga hatua hiyo kwa kuwaondoa Esperance Sportive de Tunis kwa ushindi wa jumla wa 1-0 katika hatua ya robo fainali, wakipata nafasi ya kukutana na Al Ahly kwenye mechi ya kwanza ya Nusu Fainali itakayochezwa Jumatatu, Aprili 19, huko Pretoria.

Al Ahly, ambao wameweka rekodi ya kutinga Nusu Fainali mara sita mfululizo, wameendelea kuimarisha ubabe wao katika soka la Afrika kwani katika changamoto ya CAF msimu huu wamejipatika Clean Sheets 12 katika michezo 14 chini ya uongozi wa kocha Marcel Koller ambaye hajawahi kupoteza mchezo katika hatua za mtoano.

Katika upande mwingine, AS FAR Rabat wametolewa nje ya mashindano na Pyramids FC kwa jumla ya magoli 4-3 katika michezo yote miwili.

Katika hatua ya Nusu Fainali, Pyramids wao wamepangwa kukutana na Orlando Pirates au MC Alger.