Al Masry Yawasili Dar Es Salaam Kuwakabili Simba SC
Kwa mujibu wa wasemaji wa klabu hiyo, Al Masry iliamua kufika mapema Dar es Salaam ili kuanza maandalizi ya hali ya juu ya mchezo huo.
HABARI ZA MICHEZO
4/7/2025


Timu ya Al Masry ya nchini Misri tayari imefika jijini Dar es Salaam tayari kukutana na Simba SC katika mechi ya mkondo wa pili ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho CAF. Mechi hii imevutia macho ya mashabiki wa soka nchini kutokana na umuhimu wake kwa timu zote mbili.
Kwa mujibu wa wasemaji wa klabu hiyo, Al Masry iliamua kufika mapema Dar es Salaam ili kuanza maandalizi ya hali ya juu ya mchezo huo.
Timu ya Al Masry ya nchini Misri tayari imefika jijini Dar es Salaam tayari kukutana na Simba SC katika mechi ya mkondo wa pili ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho CAF. Mechi hii imevutia macho ya mashabiki wa soka nchini kutokana na umuhimu wake kwa timu zote mbili.
Kwa mujibu wa wasemaji wa klabu hiyo, Al Masry iliamua kufika mapema Dar es Salaam ili kuanza maandalizi ya hali ya juu ya mchezo huo. “Hii ni fursa ya kipekee ya kuonyesha uwezo wetu katika jukwaa la kimataifa, na tuko tayari kukabiliana na changamoto zitakazotupata dhidi ya Simba,” alisema msemaji wa klabu, akiwa anataja umuhimu wa maandalizi haya katika kuhakikisha mafanikio ya timu.
Mashabiki wa Al Masry wamekuwa wakifuatilia maandalizi ya timu yao hatua kwa hatua, huku wakisubiri kwa shauku mechi hii itakayoimarisha hadhi ya timu yao katika mashindano ya CAF.
Msimamo huu wa klabu unachukuliwa kama hitaji la kusonga mbele katika historia ya mchezo hususani mashindano ya kimataifa, ambapo ushindani kati ya timu kutoka bara la Afrika umeimarika zaidi kuliko hapo awali.
Kwa upande mwingine, Simba, ambayo imekuwa ikionesha ubora katika soka la ndani na kimataifa, inatarajia kufanya makubwa katika mechi hii, na kupambana kufa na kupona ili kusonga mbele katika hatua inayofuata ya mashindano hayo.
Katika mchezo huo, Al Masry wanahitaji ushindi, sare ya aina yoyote, au kutokupoteza kwa magoli kuanzia mawili ili wafuzu hatua inayofuata, kutokana na ushindi wao wa magoli mawili kwa bila walioupata katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua hiyo muhimuz huku Simba wao wakihitaji kufanya kila linalowezekana ili wapate ushindi usipungua magoli matatu.
Mashabiki wa soka nchini, na Afrika kwa ujumla watakuwa macho, wakiangalia jinsi klabu hizi zitakavyoshindana kwenye mechi hii ya kusisimua ya Kombe la Shirikisho CAF.


“Hii ni fursa ya kipekee ya kuonyesha uwezo wetu katika jukwaa la kimataifa, na tuko tayari kukabiliana na changamoto zitakazotupata dhidi ya Simba,” alisema msemaji wa klabu, akiwa anataja umuhimu wa maandalizi haya katika kuhakikisha mafanikio ya timu.
© 2024. All rights reserved.
Wasiliana Nasi
Tafadhali tujulishe kuhusu maswali au maoni yako
Vigezo na Masharti vitazingatiwa kwa ofa zote na bonasi zitakazotangazwa kwenye tovuti hii. Tembelea kampuni ya betting husika kwa maelezo zaidi. Sisi sio kampuni ya betting/mikeka na hatuchukui dau zozote. Odds za kipekee tunazotoa katika makala mahususi za habari ni za burudani na hazipatikani kwa kuwekewa dau. Kutumia taarifa yoyote inayopatikana katika www.mkekabetting.com kukiuka sheria yoyote ni marufuku. Angalia kanuni za bahati nasibu mtandaoni katika eneo lako la mamlaka kabla ya kuweka dau zozote na viungo vyovyote vya kutangaza mikeka.
Beti Kistaarabu
Hairuhusiwi chini ya miaka 18

